Saa hii, kuna hatua ya baraza na wewe mwenyewe 2 Mgeni (wageni) na 3 mwanachama (s) ambayo juu ya Hatua.
Mwanachama (wanachama) pamoja na wanachama wa Awqaf. kuona ni nyingine mbunge (s) online na wewe click Kubonyeza Hapa
Tafuta
Lugha
Mabadiliko ya lugha mbalimbali::
Categories Menu
Hakuna bidhaa sasa hivi kwa ajili ya kuzuia hili.
Sanduku Kuingia
Hawana akaunti bado? Unaweza kujenga mmoja. Kama Mtumiaji aliyesajiliwa unaweza kuwa na baadhi ya faida kama meneja wa mandhari, comments Configuration na maoni post kwa jina yako.
Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid
Imetarjumiwa na Ummu Ummu Ayman..
Ili kusaidia familia za Kiislam na kueneza mafundisho ya Uislam katika kujenga
familia, MSA (Muslim Students Association) katika Chuo Kikuu cha Alberta,
Canada, kimetayarisha ufupisho wa tafsiri ya vitabu viwili. Vitabu katika lugha
ya kiarabu vilivyotungwa na Shaykh Muhammad 'Abdul-Haliym Haamid. Mwanachuoni wa
Kimisri, ambaye amemaliza masomo yake katika chuo cha Islamic University cha
Madiyna An-Nabiwiyyah huko Saudi Arabia. Vitabu vyenyewe ni :
1. Namna ya kumfurahisha Mkeo
2. Namna ya kumfurahisha Mumeo
Hivi ni vitabu vizuri kabisa vya Kiarabu ambavyo tumeviona katika
somo hili. Vimekwenda mbali katika kuelezea, kuanzia haki
na wajibu mpaka adaab (tabia njema) na kwenda mbali katika
kutekeleza haki hizi katika maisha ya kila siku. Ufupisho ufuatao unamulika
zaidi katika majukumu ya nini kinaweza au kinachotakiwa kifanywe. Kila jambo
lililotajwa na muandishi limeegemezwa katika ushahidi wa Qur-aan, Sunnah au
matendo ya Maswahaba, bali ushahidi haukuwekwa katika tafsiri hii. Ifuatayo ni
tafsiri ya kitabu cha kwanza.
Imefasiriwa Na: Ummu Ahmad MANUFAA KATIKA NDOA 1. Kupata kizazi ambacho kwanza kitasaidia katika ujengaji wa jamii, pili kueneza jinsia ya watu wa kila kabila au mataifa mbali mbali, na kubwa zaidi ni kuongeza idadi ya kizazi cha jamii ya kiislamu. 2. Kumridhisha Allaah (Subhaanahu Wa Ta’ala) na Mtume Wake (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam), kwa kueneza idadi ya wafuasi wa dini ya Kiislamu. Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema katika hadithi sahihi: “Oeni wake wema muwapendao na wataowapatia kizazi chema, kwani siku ya Qiyaamah nitajivunia ukubwa wa umati wangu.” [Ahmad] 3. Kupata baraka za mtoto mwema ambaye atakayemsomea dua mzee wake (atakapofariki). Maneno haya yamethibitishwa na Hadiyth maarufu inayosema kuwa: “Binaadamu anapokufa, basi ‘amali zake nzuri hukatika au humalizika, isipokuwa mambo matatu makuu nayo ni: Sadaka yenye kuendelea, Elimu yenye kunufaisha na Mtoto mwema atakayemuombea du’aa mzee/wazee wake.” [Riyadhus-Swaalihiyn] Faida nyenginezo zipatikanazo katika ndoa ni:
Kwanza kabisa, ijulikane wazi kwamba kusudio la makala hii si kutoa fatwa wala hukumu. Lengo ni kuweka wazi manufaa na madhara ya Facebook ili mtu binafsi atoe hukumu yake mwenyewe. Je, ni Facebook au Fitnabook? Hili ni suali ambalo watu wengi wameanza kujiuliza baada ya kujionea vitimbi na kashfa kadhaa katika huu mtandao ambao unazidi kujipatia umaarufu kila pembe ya dunia. Naam, kuna vitimbi kadhaa vinafanyika kwa jina la Facebook. Na ndio kuna vijana wengi ambao wametumbikia katika janga la fitna katika Facebook lakini nini suluhisho la hili? Kabla hatujatazama hebu kwanza tuangalie manufaa na madhara ya Facebook.
((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli wanawake, na wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake, na wanyenyekevu wanaume na wanyenyekevu wanawake, na watoao sadaka wanaume na watoao sadaka wanawake, na wanaofunga wanaume na wanaofunga wanawake…)) [Al-Ahzaab:35]
Tabia Za Mwenendo Wa Kiislamu Imeandikwa Na ‘Abdur-Rahmaan A. Ash-Shiiha Imetafsiriwa Na ‘Abdun-Naaswir Hikmany Imechukuliwa Kutoka Kitabu Cha Mwandishi “Ujumbe Wa Uislamu.”
Tabia Za Mwenendo Wa Kiislamu
Shari’ah ya Kiislamu imeasisi na kulingania ustaarabu mbali mbali wa jamii. Wakati huo huo, imetahadharisha kuwepo adhabu siku ya Qiyaamah pindipo mtu atakaposhindwa kushikamana na Shari’ah hizo. Imaam Muslim amepokea kwamba Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) amesema: ((Je munamjua nani muflisi?)) Walijibu: ((Muflisi miongoni mwetu ni yule ambaye hana pesa wala mali.)) Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) akasema: ((Muflisi ndani ya ummah wangu ni yule anayekuja siku ya Qiyaamah akiwa na Swalah, Zakaah na Swawm, hata hivyo alikuwa akivunjia heshima, kusengenya, kutukana na kuwapiga wengine.
Yaliyokuwa Sunnah Na Bid'ah Katika Sherehe Za 'Iyd
BismiLLaahi wa AlhamduliLLaah wa swalaatu wa salaam 'alaa RasuliLLaah Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa aswahaabihi wa sallam.
“Kwa kila jamii ya watu kuna sikukuu, na hii ‘Iyd ndiyo sikukuu yetu” alisema Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam) kumwambia Abu Bakr (Radhiya Allaahu ‘anhu). [Al-Bukhaariy na Muslim].
Mwenyezi Mungu Anatusimulia moja ya visa vilivyomo katika Qur-aan Tukufu:
"Na Maryam mtoto wa 'Imraan aliyejihifadhi nafsi yake na Tukampulizia humo roho Yetu (inayotokana na Sisi), na akayasadikisha maneno ya Mola wake, na Vitabu Vyake; na alikuwa miongoni mwa wanyenyekevu (wakubwa)." (Suratu at-Tahrym: 12)
Ndugu zangu Waislam, katika kalenda ya Hijri (Kalenda ya Kiislam) imeanza, na kwa ajili hiyo tutajikumbusha kidogo juu ya umuhimu wa siku hizi kwa ajili ya kuelewa umuhimu wake na kwa ajili ya kujifunza angalau machache juu ya Hijrah ya Mtume wetu mtukufu Muhammad (Swalla Llaahu ‘alayhi wa sallam) pamoja na Maswahaba wake watukufu (Radhiya Llaahu ‘anhu).
Mwaka jana katika mnasaba huu, tulisoma namna gani tukio la Hijrah lilivyokuwa muhimu kupita matukio yote yaliyopata kutokea katika historia ya Kiislam, na hii ni kwa sababu kutokana na Hijrah, taifa la mwanzo la Kiislam liliweza kuundwa, na Waislamu wakaweza kuweka miguu yao juu ya ardhi, madhubuti kwa ajili ya kuisimamisha dini yao, kuilinda itikadi yako, na kuweza kuieneza ulimwenguni kote.
Makosa Ya Msingi Yaliyomo Ndani Ya Katiba Ya Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Kwa Mtazamo Wa Uislamu
Isbaal ni urefushaji wa kitu na makusudio hapa katika makala hii ambayo itazungumzia vazi la mwanamme, makusudio yake kishari’ah ni kuvaa kivazi chochote chenye kuvuka chini ya mafundo ya miguu kwa mwanamme; iwe ni kikoi, shuka, kanzu, joho au suruali. Nalo ni jambo lenye kukatazwa na limeharamishwa kwa nuswuus (maandiko) mbalimbali ya kishari’ah kutoka katika Hadiyth za Mtume (Swalla Allaahu ‘alayhi wa aalihi wa sallam).
Hapa chini tutaona hoja au madai tata za wanaotetea kuburuza/ kuburura nguo na majibu dhidi ya madai hayo.
Hoja Mojawapo: Kuwa Isbaal Inawahusu Wenye Kuvaa Kwa Kiburi Au Kwa Fakhari Tu
Baadhi ya watu wanarukhusu Isbaal kwa kudai kuwa makatazo yaliyokuja katika Hadiyth mbalimbali ni kwa wale tu wanaovaa kwa kiburi au kujifakharisha. Ima kwa wale wanaovaa tu bila kukusudia kiburi basi inafaa na hakuna ubaya wowote.
((Ogopeni Siku Ambayo Mutarudishwa Kwa Allaah Kisha Kila Nafsi Italipa Kila Lile Ililochuma Na Wao Hawatadhulumiwa)) (Al-Baqarah: 281)
Utangulizi
Shukrani zote Anastahiki Allaah, Mola wa walimwengu wote. Swalah na amani ziwe juu ya aliyetumwa awe ni Rehma kwa ulimwengu wote Mtume Muhammad Mtume صلى الله عليه وآله وسلم Ahli zake, Swahaba na wale ambao wamefuata Sunnah zake mpaka siku ya mwisho.
Kwa jina la Allaah, Mwingi wa Rehma, Mwenye Kurehemu
Katika usiku wa giza, Abu Lu’lu’ Al-Majuusi alijificha katika vivuli akijiandaa kwa ajili ya Swalaah ya Alfajiri, wakati ambapo ataendesha mipango yake ya kishetani kumuua Amiyr wa waumini – ‘Umar bin Al-Khattwaab (Radhiya Allahu ‘anhu).
Kulingana na Kamusi ya Kiingereza ya Collins, kazi imefafanuliwa kama juhudi za kimwili au kiakili zilizoelekezwa kufanya/ kutengeneza kitu, malipo anayopewa kwa amali, biashara, utaalamu, shughuli au ufahamu.
Kuzuru Msikiti wa Mtume صلى الله عليه وآله وسلم au kuweko Makkah kufanya 'Umrah (kwa Wanaofanya Hajjut-tamattu'u) na kuendelea kuswali hapo Masjidul-Haraam.