Saa hii, kuna hatua ya baraza na wewe mwenyewe 2 Mgeni (wageni) na 3 mwanachama (s) ambayo juu ya Hatua.
Mwanachama (wanachama) pamoja na wanachama wa Awqaf. kuona ni nyingine mbunge (s) online na wewe click Kubonyeza Hapa
Tafuta
Lugha
Mabadiliko ya lugha mbalimbali::
Categories Menu
Hakuna bidhaa sasa hivi kwa ajili ya kuzuia hili.
Sanduku Kuingia
Hawana akaunti bado? Unaweza kujenga mmoja. Kama Mtumiaji aliyesajiliwa unaweza kuwa na baadhi ya faida kama meneja wa mandhari, comments Configuration na maoni post kwa jina yako.
Msamaha Na Ujira Mkubwa Tutakaopata Baada Ya Kuzichuma Sifa Kumi Njema
Baada kukumbushana maneno ya Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) katika Aayah tukufu
iliyotaja sifa kumi njema, tumeona kwamba mwisho kabisa Allaah (Subhaanahu wa
Ta'ala) Anasema:
((أَعَدَّ اللَّهُ لَهُم مَّغْفِرَةً وَأَجْرًا عَظِيمًا))
((Allah Amewaandalia msamaha na ujira mkubwa)) [Al-Hazab:35]
Vile vile Anasema katika Aayah nyingine:
((وَعَدَ اللّهُ الَّذِينَ آمَنُواْ وَعَمِلُواْ الصَّالِحَاتِ
لَهُم مَّغْفِرَةٌ وَأَجْرٌ عَظِيمٌ))
((Allah Amewaahidi waliomuamini na wakatenda mema kwamba watapata maghfira na
malipo makubwa)) [Al-Maaidah]
Maana kwamba;
Tutasamehewa Madhambi yetu ambayo hakuna aliyeepukana nayo, lakini Mola wetu ni
Mkarimu Mwingi Wa Kurehemu na Mwingi wa Msamaha Hukubali toba zetu wakati wowote
kama Anavyotuahidi katika Qur-aan na pia katika Hadiyth za Mtume (Swalla Allahu
'alayhi wa aalihi wa sallam):
Shaykh 'Abdullaah 'Adhamiy
Imefasiriwa na Iliyaasa
Muenzi Mke Wako
Kwa kuoa huchukui tu mke, Bali unachukua ulimwengu wako mzima. Kuanzia hapo
mpaka maisha yako yote mke wako atakuwa mwenzio, mwandani wako, na rafiki yako
mpenzi.
Atashiriki katika nyakati zako nzuri, siku zako, na miaka yako. Atakuwa pamoja
nawe katika furaha na shida, katika mafanikio na tabu, katika ndoto zako na
katika wakati wa hofu. Ukiumwa, atakupa huduma bora kabisa. Wakati unapohitaji
msaada atafanya vyovyote awezavyo kwa ajili yako. Wakati una siri, ataitunza
siri yako, wakati unahitaji ushauri, atakupa ushauri mzuri kabisa.
Atakuwa na wewe utakapoamka asubuhi kitu cha kwanza ambacho macho yako yataona
ni macho yake.
Wakati wa mchana, atakuwa na wewe, kama kuna wakati mchache
hatokuwa na wewe kwa kimwili, atakuwa anakufikiria wewe, anakuombea dua kwa moyo
wake wote, akili yake yote, na roho yake nyote. Ukienda kulala usiku, kitu cha
mwisho macho yako kuona itakuwa ni yeye, na ukilala bado utakuwa unamuona katika
ndoto zako. Kwa kifupi atakuwa ni ulimwengu wako mzima na wewe utakuwa ulimwengu
wake mzima.
رسالة إلى المرأة: Ujumbe Kwa Mwanamke 'Allaamah Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan Mfasiri: Abu Bakr Khatwiyb al-Atrush
Bismi Allaahi Ar-Rahmaani Ar-Rahiym. Alhamdu Allaahi Rabil 'Aalamiyn. Swalah na salaam zimwendee Mtume wetu Muhammad (swalla Allaahu 'alayhi wa sallam) na ahli zake na Maswahaba wake kwa jumla (radhiya Allaahu ´anhum). Tumesikia kwenye hizi khutbah mbili zenye baraka khayr nyingi kutoka kwa Khatwiyb wetu - Allaah Ampe mafanikio. Kazungumzia masuala ya khatari, nayo ni masuala ya mwanamke. Mwanamke enyi ndugu! Allaah Kamuumba kwa lengo kubwa katika maisha haya, kama Alivyomuumba mwanaume. Na kila mmoja ana umuhimu [kazi] Yake. Mwanaume ana kazi yake na mwanamke ana kazi yake. Kila mmoja akishikamana na kazi yake na kuitimiza, jamii itafikia khayr kubwa. Na ikiwa nidhamu itayumbishwa, ndiyo kunatokea kasoro nyingi. Kama mlivyosikia jukumu la mwanamke wakati wa Ujaahiliyyah (kabla ya kuja Uislamu), na jukumu lake leo kwenye miji ya kikafiri na kwa Waislamu wenye misimamo.
((Hakika Waislamu wanaume na Waislamu wanawake, na Waumini wanaume na Waumini wanawake, na watiifu wanaume na watiifu wanawake, na wasemao kweli wanaume na wasemao kweli, wanaosubiri wanaume na wanaosubiri wanawake ….)) [Ahzaab:35]
Sifa zote kamilifu njema anastahiki Allah Aliyetukuka Mola Mlezi wa wa walimwengu wote ambaye hana mshirika katika Ufalme Wake. Swalah na salamu zimshukiye kipenzi chetu Muhamad (Swala Allaahu 'alayhi wa sallam) ahli zake, sahaba zake (Radhiya Allaahu 'anhum) na watangu wema mpaka Siku ya Mwisho.
Ishara ya “NIKE” ikiwa ni kwa alama kama ya kupata kama ilivyo hapo juu au kwa neno lenyewe la “Nike” ambalo hutumiwa mara nyingi kuwekwa kwenye nguo za kuvaa au kwenye viatu vya michezo na mazoezi. Waislamu tunatakiwa kujiepusha kununua bidhaa hii, vile vile tujiepushe na kuivaa kwa wale ambao tayari wameshakuwa nayo majumbani.
Motone kadhaa ya mafuta ya Habbat-Sawdaa yaliotiwa kwenye maziwa ya moto na asali; humaliza asidi.
Uvimbe Wa Tumbo
Atachukuwa unga wa Habbat-Sawdaa kiasi cha kijiko kimoja na kijiko cha urkusus (licorice) hivyo atavichanganya na juisi ya pea iliotengenezwa pamoja na kokwa zake; halafu anywe; ataona nafuu kubwa.
Matumizi Ya Kunufaisha Ya Habbat-sawdaa-2 (habba Soda - Chembe Nyeusi ) Sunnah - Siyrah
(Itumieni habba hii, hakika ndani yake muna shifaa (ponyo) ya kila aina ya ugonjwa isipokuwa mauti)). (Al-Bukhaariy)
Kunyonyoka Nywele
Ataukanda unga wa Habbat-Sawdaa katika juisi ya chirichiri pamoja na kijiko cha siki nyepesi na kikombe cha mafuta ya zeituni, halafu asugue kichwani kwa mafuta hayo kila siku jioni pamoja na kukiosha kichwa kwa maji na sabuni kabla ya kupaka.
Kwa hakika kila sifa njema ni Zake Allaah, tunamtukuza Yeye, na tunamtaka msaada Yeye na tunamuomba msamaha Yeye. Tunajilinda kwa Allaah kutokana na maovu ya nafsi zetu na udhaifu wa vitendo vyetu. Aliyeongozwa na Allaah hakuna wa kumpoteza na aliyepotezwa na Allaah hakuna wa kumuongoza. Nashuhudia kuwa hapana apasaye kuabudiwa kwa haki ila Allaah na nashuhudia kuwa Muhammad ni mja Wake na Mtume Wake.
BismiLlaahi Rahmaanir Rahiym Shukrani ni za Allaah na rehma na amani zimfikie Mtume wa Allaah na watu wake na Maswahaba zake na wanaowafuata hadi Siku ya mwisho.
Amma ba’ad;
Hakika furaha ni utulivu wa mioyo yetu, ni kipumbazo cha macho yetu. Wakati tunaposikia habari ya ‘Arusi (Harusi) kuwa fulani anamuoa fulani, jambo hili ni sababu ya kusimamisha (Sunnah) mwendo Aliouweka Mola na kwa njia hii ndio kuendelea kizazi cha viumbe.
Fataawa Za Wanachuoni Kuhusu Mavazi Ya Mwanamke ‘Arusini Na Wanapokuwa Na Wanawake Wenzao
Swali:
Nini shari'ah ya kiislamu kwa wanawake kuvaa nguo za wazi kabisa wanapohudhuria harusi, Kama kanzu fupi zinazoonyesha miguu au mikono yote kuwa wazi au kuvaa bega na moja liko wazi, baadhi ya au kifua kuwa wazi, au kanzu kumbana (tight) hadi mwili wote viungo vyake vinaonekana, au mgongo kuwa wazi n.k.. Je inaruhusiwa kwa vile wako mbele ya wanawake wenzao? ipi mipaka ya mavazi baina Yao?
Kauli Za Maimaam Wanne Kuhusu Kushikamana Na Sunnah Na Kuacha Kufuata Rai Zao
Imefasiriwa na Abu 'Abdillaah Muhammad Baawazir kutoka kitabu cha: 'Swiffatus-Swalaatin-Nabbiy (Sifa ya Swalah ya Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) kilichoandikwa na Shaykh Al-Albaaniy (Rahimahu Allaah)
Itakuwa ni manufaa makubwa ikiwa tutazieleza baadhi ya kauli zao hapa, kwani labda hii itamuonya mtu au itawakumbusha wale ambao wanafuata rai za Maimaam au madhehebu maalum, bali wanaofuata kwa upofu wale Waalimu au Mashaykh na wale walio chini ya daraja ya hao Maimaam wanne wakubwa[1]wakishikilia madhehebu yao au rai zao kama kwamba zimeteremeshwa kutoka mbinguni! Na hali Allaah (Subhaanahu wa Ta'ala) Anasema:
Kuachilia ndevu ni wajibu kwa wanaume kwa dalili zifuatazo: 1- Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam) ameamuru kuziachilia. Amri hii ni ya lazima, kwani hakuna kiashirio chochote kinachoigeuza na kuipeleka katika usunnah. Na kati ya amri hizo ni neno lake Mtume (Swalla Allaahu 'alayhi wa aalihi wa sallam):
Makos Tanayohusu Twawaaf, Sa'y, Yanayotendeka Minaa, Katika Kisimamo Cha 'Arafah, Katika Eneo La Muzdalifah, Katika Sehemu Za Kurushia Mawe Kuzuru Kaburi La Mtume
Mahujaji wengine wanavuka kituo kilichoteuliwa kwa ajili ya ihraam katika njia za msafara wao bila ya kuwa katika hali ya ihraam au bila ya kuwa katika ihraam hapo. Wanaendelea hadi wanafika Jiddah au sehemu nyingine katika mipaka ya vituo ambako huko ndio wanaingia katika hali ya ihraam.
Kila sifa njema ni zake Mwenyezi Mungu Mola wa viumbe vyote, sala na amani ziwe juu ya Imamu wa Mitume, Nabii wetu Muhammad, na jamaa zake, na Masahaba wake wote.
Ama baada:_
UISLAMU:_ ni kushuhudia kuwa hapana Mola apasae kuabudiwa kwa haki ila Mwenyezi Mungu mmoja, na Muhammad (rehema na amani za Mwenyezi Mungu ziwe juu yake) ni mjumbe wa Mwenyezi Mungu, (kushuhudia) kwa moyo, na kwa ulimi, na kwa viungo.
Na (huo Uislamu) unajumuisha kuamini nguzo sita za Imani kwa kutekeleza nguzo tano za Uislamu, na nguzo mbili za Ihsani.